Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Tovuti ya habari ya Muungano wa Vijana wa Mapinduzi ya 14 Februari imetangaza kuwa utawala wa Aal Khalifa, siku ya Jumatano tarehe 9 Julai 2025 (18 Tir 1404), ulimkamata Hussein Farid Al-Jazairi, mkazi wa mji wa Zahra, kwa kuchapisha maudhui ya kuunga mkono misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni, kupitia jukwaa la Instagram.
Mwanaharakati huyu wa mitandao ya kijamii, baada ya kukamatwa, alipelekwa kwanza katika ofisi ya mwendesha mashtaka, na kisha aliamriwa kuwekwa kizuizini kwa muda wa wiki moja kwa ajili ya kuendeleza uchunguzi, na hivyo kupelekwa jela.
Hatua hii inachukuliwa huku taasisi za haki za binadamu zikiwa tayari zimekosoa mara kadhaa sera ambazo zinakandamiza uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hasa kuhusu misimamo ya kisiasa inayochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Maoni yako